Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Msonde awataka walimu wasifanye kazi kwa mazoea

Dk Msonde akizungumza na wadau mbalimbali wa Elimu wakati akifunga mafunzo ya MEWAKA

What you need to know:

  • Dk Charles Msonde amewataka walimu kuacha kufanya kazi kwa mazoea sambamba na kulinda maadili ya utumishi wa umma.

Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia elimu, Dk Charles Msonde amewataka walimu kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwa sababu kwa sasa watapimwa kulingana na matokeo.

 Msonde ameyasema hayo wakati wa kufunga mafunzo rejea kwa viongozi na waratibu wa Mafunzo Endelevu ya Walimu Kazini (Mewaka) yaliyokuwa yakifanyika mkoani Morogoro kuanzia Januari 28, 2023.

Pia, Msonde amewataka walimu kulinda maadili ya utumishi wa umma huku uwajibikaji ukiendana na Sheria, Kanuni na Miongozo inayotolewa na Serikali.

“mafunzo haya yamelenga kujenga uwezo wa walimu ili wakirudi kwenye utendaji kazi wao tuone wakitekeleza majukumu yao kwa weledi na kama tutabaini changamoto yeyote tutaendelea kuitafuta katika mafunzo yatakayofuata,” alisema.

Pia ameelekeza kila kata kuwa na kituo cha walimu na kuwa pale ambapo hakuna kituo basi ichaguliwe shule yoyote ya msingi au sekondari na iwe ni kituo cha walimu na walimu lazima wawe na uwezo wa kubainisha matatizo shida na changamoto zao za kitaaluma na wawezeshwe.

Mafunzo haya yaliyofanyika kwa siku mbili yamehusisha washiriki 286 wakiwemo maafisa elimu wa halmashauri na waratibu wa Mewaka ngazi ya halmashauri, wadhibiti ubora wa shule wilaya, Makatibu Wasaidizi wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), na wakufunzi kutoka vyuo vya ualimu.