Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kigogo wizarani alimwa faini Sh2.9 milioni

What you need to know:

  • Aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Easter Riwa amehukumiwa kulipa faini ya Sh2.9 milioni au kwenda jela mwaka mmoja baada ya kukutwa na hatia ya kufanya ubadhirifu wa fedha za wizara hiyo.

Dar es Salaam. Aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Easter Riwa amehukumiwa kulipa faini ya Sh2.9 milioni au kwenda jela mwaka mmoja baada ya kukutwa na hatia ya kufanya ubadhirifu wa fedha za wizara hiyo.

Pia mahakama hiyo imemuamuru mshtakiwa huyo kurudisha kiasi cha Sh 2.9 milion kwenye wizara hiyo zilizotakiwa kulipa posho za maofisa wa maendeleo ya vijana mkoani Ruvuma.

Hukumu hiyo imetolewa Leo Jumatatu Januari 30, 2023 na Hakimu Mkazi mkuu, Pamela Mazengo aliyesema mshtakiwa ametiwa hatiani kwa mashtaka 21 Kati ya hayo 19 ya kughushi, moja la ubadhirifu na moja la kutumia nyaraka za uongo kumdanganya mwajili wake.

Mazengo amesema mashtaka 19 ya kughushi kila moja anatakiwa alipe faini ya Sh100,000 au kwenda jela mwaka mmoja, huku shitaka la ubadhirifu akitakiwa alipe faini ya Sh500,000 au kwenda jela mwaka mmoja na shitaka la kutumia nyaraka za uongo kumdanganya mwajiri wake mshtakiwa huyo anatakiwa kulipa fidia ya Sh500,000 au kwenda jela mwaka mmoja.

Amesema mshitakiwa huyo akimaliza kifungo chake anatakiwa ailipe Wizara hiyo Sh2.9 milioni fedha kwa ajili ya malipo ya posho za maofisa wa maendeleo ya vijana wa mkoani Ruvuma ambazo.

"Mshitakiwa anatakiwa kulipa fidia kwa kila kosa ambapo jumla yake ni Sh2.9 milioni na kila kosa anatakiwa afungwe mwaka mmoja lakini vyote vitakwenda kwa pamoja ambapo kifungo chake no mwaka mmoja," amesema Mazengo.