Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

RC Pwani atahadharisha wakuu wa wilaya wapya migogoro ya ardhi

Mkuu wa Wilaya ya Mafia  Zephania Sumaye  akiapa kushika nafasi hiyo leo Jumatatu January 30,2023 kulia aliyekaa chini ni Mkuu wa Wilaya ya Kibiti kanari Joseph Kalombo,Picha na Sanjito Msafiri

What you need to know:

  • Changamoto ya migogoro ya ardhi ambayo imeendelea kuukabili Mkoa wa Pwani  siku hadi siku ni miongoni mwa maagizo yaliyosisitizwa na Mkuu wa Mkoa huo Abubakari Kunenge kwa wakuu wa Wilaya wapya mara baada ya kuwaapisha leo Jumatatu Januari 30, 2023 Mjini Kibaha.

Kibaha. Changamoto ya migogoro ya ardhi ambayo imeendelea kuukabili Mkoa wa Pwani siku hadi siku ni miongoni mwa maagizo yaliyosisitizwa na Mkuu wa Mkoa huo, Abubakari Kunenge kwa wakuu wa Wilaya wapya mara baada ya kuwaapisha leo Jumatatu Januari 30, 2023 Mjini Kibaha.

Wakuu hao wapya wawili akiwemo Kanali Joseph Kolombo wa Kibiti na Zephania Sumaye ambaye amepangiwa Wilaya ya Mafia ni miongoni mwa wateule wa Rais walioteuliwa hivi karibuni.

"Migogoro ya ardhi ni miongoni mwa changamoto zilizopo maeneo mbalimbali kwenye Mkoa wetu hivyo ni wajibu wenu kwenda kuliangalia hilo," amesema.

Mbali na agizo hilo, Kunenge amewataka wakuu hao wa Wilaya kushughulikia kero za wananchi ikiwemo huduma za upatikanaji maji na umeme kwani lengo la Serikali ni kuhakikisha jamii inaishi kwa amani.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani, Mwishehee Mlao amesema kuwa ili utendaji wa viongozi hao uwe wa kutukuka wana wajibu wa kutumika kwa wanachi na si kinyume na hivyo.

"Mmepewa kazi na Mheshimiwa Rais mmeaminika ili imani yenu ionekane mnapaswa kuwatumikia wananchi," amesema.

Shehe wa Mkoa wa Pwani, Khamisi Mtupa amesema kuwa utendaji kazi wanaopaswa kuzingatia viongozi hao ni kujinyenyekeza kwa wananchi wanaowaongoza na ziadi ni kujali changamoto zao na kuzifanyia kazi.