Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CCM yamwagiza Waziri wa Kilimo kutatua mgogoro Kilosa, Mvomero

What you need to know:

  • Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amemtaka Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kwenda Kilosa ndani ya siku saba kutatua changamoto ya mashamba yaliyofutiwa na kurejeshwa kwa wananchi, lakini upatikanaji wake kwa ajili ya wakulima umekuwa tatizo.

Morogoro. Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amemtaka Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kwenda Kilosa ndani ya siku saba kutatua changamoto ya mashamba yaliyofutiwa na kurejeshwa kwa wananchi, lakini upatikanaji wake kwa ajili ya wakulima umekuwa tatizo.

 Chongolo ameeleza hayo leo Jumatatu Januari 30, 2023 wakati akizungumza na wananchi wa Mvumi wilayani Kilosa mkoani hapa katika mwendelezo wa ziara yake ya siku tisa katika mkoa Morogoro akiambatana na baadhi ya viongozi wa sekretarieti ya CCM.

" Lalamiko lenu ni mashamba, mmesema yapo yaliyorudishwa  lakini namna yanavyotumika. Sasa naagiza waziri apite huku kuzungumza nanyi ili kuweka utaratibu mzuri kwa ajili ya kufanya shughuli zenu za kilimo katika mashamba haya.
"Hii ndio kazi ya watendaji ya viongozi kwa sekta mbalimbali kila mmoja awajibe katika sekta yake kwa kuwapa majibu wananchi. Leo napita lakini ndani ya wiki moja niwahakikishie waziri mwenyewe atakuja kuwapa majibu kuhusu hili," amesema Chongolo.
Chongolo ameongeza kuwa," Nyinyi mmeniambia kuna mashamba na mnachotaka fursa ya kuyatumia na yeye (Bashe), ndio mhusika wa masuala yote haya, lakini hapa kuna skimu ya umwagiliaji na Serikalini imeleta fedha kwa ajili ya kuijenga," amesema.
Chongolo amesema Serikali imeweka kipaumbele kikubwa katika kilimo ikiwemo kutoa ruzuku katika mbolea ili wananchi kuipata kwa urahisi.
Amesema Serikali  imetoa ruzuku ya pembejeo katika tumbaku, korosho, pamba na mazao mengine ya kimkakati.
Katibu Mkuu huyo, amefafanua kuwa Serikali imepelekwa fedha nyingi za kujenga skimu ya umwagiliaji nchi nzima, ikiwemo wilaya ya Kilosa.
Hata hivyo, skimu hazitafanikiwa endapo, zitaachwa kuendeshwa kwa mfumo wa awali.

"Lazima tukubaliane ili skimu ziwe na tija lazima kuwepo na mameja watakaozisimamia ili kuondosha utaratibu wa kukodisha mashamba au maeneo kwa wananchi. Badala yake waweke ndani ya skimu kuwekwe utaratibu mzuri wa usimamizi wa mameneja," amesema.
Kutokana na hilo, Chongolo ameitaka wizara ya kilimo kuweka mameneja ambao ni wataalamu wa ufundi na usimamizi wa skimu hizo na si vinginevyo. Amesema hivi sasa skimu ikisumbua mtaalamu anatoka mbali kwa ajili ya kuirekebisha.
Ameitaka wizara ya kilimo kuweka utaratibu wa kuwa na wahandisi katika wilaya zote nchini zinazohusika na kilimo hasa cha umwagiliaji kwenye mikoa mikubwa ukiwemo wa Morogoro ambao upo kwenye tano bora ya kulisha Taifa.
" Lazima kuwe na meneja au mhandisi wa mkoa atakayekuwa na jukumu la kuratibu na  kusimamia miundombinu ya umwagiliaji ya ndani ya mkoa husika. Tukifanya hivyo tutasaidia dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha fedha zinazotengwa katika skimu zinawasaidia wananchi," amesema Chongolo.
Mkazi wa Mvumi, Dafloza  Daniel amesema kero yake kubwa ni kunya'nga'nywa na shamba na  mmoja ya wawekezaji  katika Kijiji cha Msowelo na kutakiwa kulipa Sh70,000 kama anataka kufanya shughuli za kilimo.
" Nina familia na kusomesha mtoto nashindwa nifanyaje, sina kitu cha kuendeleza kilimo, shamba nililotegemea nimenya'ng'anywa ndio maana leo tumemuomba katibu mkuu (Chongolo) atusaidie ," amesema Daniel.